Subscribe For Free Updates!

We'll not spam mate! We promise.

Thursday 16 July 2015

Matokeo ya kidato cha sita 2015






                                                                  BOFYA HAPA KUONA

Tuesday 14 July 2015

Uhamisho kwa Watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa July 2015.

Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI inatangaza orodha ya Majina 4655 ya watumishi wa Umma waliohamishwa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini July 2015. Aidha orodha ya watumishi 115 ambao hawakukidhi vigezo vya kuhama nayo imetangazwa.
Maelekezo yote muhimu yapo katika barua ambayo kila mtumishi atapatiwa kupitia kwa Wakurugenzi wa Mamlaka wanazotoka.

Magufuli awatangazia kiama watendaji wabovu

Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, John Magufuli akihutubia wananchi Zakheem, Mbagara jijini Dar es Salaam


JOHN Pombe Magufuli, mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), amesema iwapo atachaguliwa kuwa rais wa Tanzania hatomuogopa mtu yeyote ambaye ataenda kinyume na utaratibu uliopagwa na serikali katika kuhakikisha maendeleo yanapatikana nchini. Anaandika Pendo Omary … (endelea).
“Ninataka niseme kwa dhati kutoka moyoni. Sitamuogopa mtu na wala sitopenda mtu wa chini aonewe. Mimi sio mkali.Ni mpole kweli. Ila nawachukia sana watendaji wa serikali wabovu. Nazungumza jua linawaka. Akiamungu nitalala nao mbele,” amesema Dk. Magufuli.
Dk.Magufuli ambaye ni Waziri wa Ujenzi, ametoa kauli hiyo leo katika viwanja vya Mbagala Zakhiemu jijini Dar es Salaam, wakati yeye na Samia Suluhu, mgombea mwenza ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano, wakijitambulisha kwa wananchi na kuwashukuru wanachama wa CCM kuwapitisha ili kupeperusha bendera ya chama hicho katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Hatua ya CCM kuufanyia mkutano huo katika eneo la Mbagala inakuja, baada ya kubaini kuwa eneo hilo ni ngome ya Chama cha Wananchi CUF, hivyo hatua hiyo itasaidia CCM kujiimarisha katika eneo hilo.
Amesema ili kuhakikisha maendeleo yanapatikana, atahakikisha anaongoza kwa kutekeleza Ilani ya CCM ambayo inasimamia masuala mbalimbali ikiwemo haki, barabara, afya, kilimo, biashara, reli na maji huku akisisitiza kuondoa kero zinazowakabili wafanyabiashara ndogondogo na madereva wa bodaboda.
“ Mwanachama wa Chadema, CCM, UDP na asiye na chama wote wanahitaji maendeleo. Sipendi nifafanue yote, ili watu wengine wasije kusema nilianza kampeni mapema. Nimekuja kujitambulisha. Jina langu ni John Pombe Joseph Magufuli, amesema Magufuli.
Kwa upande wake Samia amesema kwa ufupi kuwa, ushindi wa CCM utatokana na umoja utakaojegwa na wanachama wa chama hicho na wale ambao sio wanachama.
Awali kabla ya Magufuli kuzungumza, Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM amesema, “Rais amesema yeye alikuwa mpole, sasa tumepata mtu mkali na juzi alisema atawashughulikia watu wote wanaokwenda kinyume na utaratibu.”
Mkutano huo ambao ulihudhuliwa na Nape Nnauye, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Said Meck Sadiki, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na wabunge kadhaa wa chama hicho ulianza saa 8.45 mchana mara tu msafara wa Magufuli ulipowasili.
Msafara huo ulianzia katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), na kusindikizwa na msururu wa magari na makundi ya bodaboda huku Nnauye akiingia katika viwanja hivyo akiwa amepakizwa nyuma ya moja ya bodaboda hizo.
Pia viwanja hivyo vilivyofurika mamia ya wafuasi wa CCM, huku kukiwa na mabasi zaidi ya 70 kutoka kampuni ya usafiri ya Dar es Salaam ( UDA) na watu binafsi ambayo yametumika kuwaleta wanachama hao kutoka katika maeneo mbalimbali ya jiji.

Chadema yatoa mwongozo udiwani

Viongozi wa juu wa Chadema
                                                      Viongozi wa juu wa Chadema


HATIMAYE  Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetoa Mwongozo uliokuwa unasubiriwa kwa muda mrefu kuhusu namna ya kuendesha zoezi la kura ya maoni katika ngazi ya udiwani nchi nzima. Anaripoti Deusdedit Kahangwa …. (endelea).
Kwa mujibu wa Mratibu wa Kanda Taifa, Mohamed Mtoi, Mwongozo huo unaotaja wajumbe wa vikao vya uteuzi katani pamoja na masharti ya kisheria kuhusiana na zoezi hili, unapaswa kuzingatia na watendaji wote wa Chadema Tanzania nzima.
Kwa mujibu wa Mwongozo huo, Kamati ya Utendaji ya Kata nidyo yenye jukumu la “kufanya uteuzi wa awali wa wagombea Udiwani.” Baadaye, uteuzi huo unapaswa kuthibitishwa na “Kamati ya Utendaji ya Jimbo” husika. 
Mwongozo huo unasisitiza kwamba, ni muhimu masharti ya akidi ya vikao vya uchaguzi kwa mujibu wa Katiba ya Chadema kuzingatiwa. Kulingana na “Ibara ya 6.2.2 (b) ya Katiba ya Chama ya mwaka 2006 akidi ya Kikao cha Uchaguzi ni 75%,” inasema mwongozo.
Mbali na kutaja wajumbe wa vikao vya uteuzi, mwongozo huo umefafanua masharti ya uteuzi kwa mujibun wa Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za mitaa (Udiwani) ya mwaka 1979 (The Local Authorities (Elections) Act 1979).
Kwa mujibu wa sheria hii, chini ya Kifungu cha 39, mtu anayetaka kugombea Udiwani  anapaswa kuwa na vigezo vifuatavyo: awe raia wa Tanzania, awe ametimiza miaka 21, awe mwanachama wa Chama cha Siasa, na awe mkazi wa Halmashauri ambapo uchaguzi wa Kata unafanyika. 
Mwongozo huo umewakumbusha watendaji wa Chama kuzingatia masharti ya kifungu cha 40 cha sheria hiyo.
Kulingana na kifungu hicho, mtu atapoteza sifa za kugombea udiwani ikiwa mtu huyo ana uraia wa nchi nyingine; au mtu huyo amethibitika kuwa ana matatizo ya akili kwa mujibu wa sheria; au mtu huyo amehukumiwa hukumu ya kifo au hukumu nyingine jela zaidi ya miezi sita; au amewekwa kizuizini kwa muda unaozidi miezi sita; au ni mbia au meneja wa kampuni ambayo imeingia mkataba na Halmashauri husika ambayo yeye anagombea; au ikiwa amezuiliwa kujiandikisha kuwa mpiga kura kwa mujibu wa sheria.
Vile vile, mwongozo huo umewakumbusha watendaji hao kuzingatia masharti ya kifungu cha 42(1) cha sheria hii.
Kwa mujibu wa kifungu hiki, mgombea lazima awe na wadhamini wasiopungua kumi; lazima awasilishe tamko lililosainiwa na Hakimu kuona kuwa anazo sifa na vigezo vya kuteuliwa kugombea; na lazima awasilishe tamko la msimamizi wa uchaguzi wadhamini waliomdhamini ni wapiga kura halali wa Kata anayogombea.
Sababu za kuwasilisha pingamizi dhidi ya mgombea wa Udiwani, kama zilivyotajwa katika kifungu cha 44 cha sheria hiyo, zimegusiwa pia.
Kwa mujibu wa mwongozo huo, mgombea anaweza kuwekewa pingamizi ikiwa taarifa za mgombea zilizopo kwenye fomu ya kuomba uteuzi hazijitoshelezi kumtambulisha; au ikiwa fomu yake ya uteuzi haiendani na taratibu za kisheria za uteuzi; au ikiwa kutokana na yaliyomo kwenye fomu ya uteuzi mgombea anakosa vigezo vya kuteuliwa; au ikiwa pingamizi dhidi ya mgombea liwasilishwe kabla ya saa kumi siku inayofuata mara baada ya siku ya uteuzi. 
Utaratibu wa Kufanya Vikao vya Kura ya Maoni Katani
Kwa mujibu wa mwongozo uliotolewa na chama, utaratibu wa kufanya vikao vya kura ya maoni ngazi ya madiwani ni kama ifuatavyo:
Kwanza, Katibu wa Kata atachambua fomu za wagombea na taarifa zao kwa ajili ya kuwasilisha taarifa kwenye kikao cha Kamati ya Utendaji ya Kata. Pili, Taarifa ya Katibu wa Kata kuhusu wagombea itawasilishwa kwenye Kamati ya Utendaji ya Kata.
Tatu, Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Kata kama walivyoainishwa katika ibara ya 7.3.8 ya Katiba wataipokea taarifa hiyo. Nne, kama Mwenyekiti wa Kata ni mgombea, basi kikao kitaazimia kumteua Mwenyekiti mwingine wa muda ambaye si mgombea.
Tano, Katibu wa Kata atawasajili wajumbe wote wa kikao na watasaini karatasi ya mahudhurio.
Sita, Katibu wa Kata ataandaa karatasi za kupigia kura ya maoni zikiwa na majina ya wagombea wote, kila jina la mgombea likiwa na kisanduku cha kumwezesha mpiga kura kuweka tiki mbele ya jina la mgombea. 
Saba, Katibu Kata ataandaa fomu za matokeo zikiwa na nafasi kwa ajili ya wagombea na mawakala wao kusaini baada ya uchaguzi, ili baadaye aweze kuwasilisha fomu hizo kwa Katibu wa Jimbo wa Jimbo/Wilaya.
Nane, Katibu wa Kata ataandaa muhtasari wa kikao cha uteuzi wa mgombea udiwani na kuhakikisha unasainiwa na Mwenyekiti na Katibu wa kikao. Tisa, Katibu wa Kata atawasilisha taarifa ya uteuzi kwa Katibu wa Jimbo/Wilaya kwa ajili ya hatua zaidi.
Na kumi, Kamati ya Utendaji ya Jimbo/Wilaya itapokea, kujadili na kufanya uteuzi wa mwisho wa wagombea udiwani. 
Nyaraka zinazohitajika wakati wa uteuzi wa wagombea udiwani
Kulingana na mwongozo uliotolewa na chama, mchakato wa uteuzi wa wagombea udiwani utaongozwa na nyaraka zifuatazo: 
Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa1979; Kanuni za Uchaguzi za Mwaka 2010; Mwongozo wa Tume kwa vyama vya siasa na wagombea wa Udiwani, Ubunge na Urais; Maadili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015; Katiba ya Chama ya Mwaka 2006 Toleo la mwaka 2014; Mwongozo wa Chama Dhidi ya Rushwa; na Kanuni za Uchaguzi wa Kiserikali na ndani ya Chama kama zilivyorekebishwa mwaka 2012.
Nyaraka nyingine ni Fomu za kuomba uteuzi za wagombea wa Udiwani; Fomu za mahudhurio ya wajumbe kikao cha uteuzi/mapendekezo; Karatasi za Kura na majina ya wagombea; Karatasi za taarifa ya Matokeo; na Muhtasari wa kikao cha uchaguzi utakaoandaliwa na Katibu wa Kata na Jimbo/Wilaya.
Utaratibu wa kura za maoni udiwani viti maalum.
Vigezo vya uteuzi wa Wagombea Udiwani Viti Maalum navyo vimetajwa katika mwongozo huu. Kwa mujibu wa mwongozo huu, vigezo vya jumla vya uteuzi wa madiwani viti maalum ni ka aifuatavyo:
Kwanza, ni lazima mgombea awe mwanachama wa CHADEMA; lazima awe mwanachama wa BAWACHA;  na lazima awe amejaza fomu zitakazoandaliwa na BAWACHA Makao Makuu kwa ajili ya kuwatambua wagombea. 
Kwa mujibu wa mwongozo huo, kutakuwa na kamati ya kupitia, kuchambua na kuchuja majina ya wagombea udiwani viti maalum. 
Kamati hiyo ya mchujo itaundwa na ngazi mbili. Katika ngazi ya kwanza kutakuwepo na Sekretariati ya BAWACHA Wilaya/Jimbo. Na katika ngazi ya pili kutakuwepo na Kamati ya Utendaji ya Wilaya/Jimbo. Kamati hii itapewa vigezo kutoka ngazi ya Taifa na kila kigezo kitakuwa na alama zake kwa ajili ya kuiwezesha kamati kuwapata wagombea walio bora. 
Mwongozo huo unafafanua kwamba, idadi ya Viti Maalum katika Halmashauri husika itategemea maelekezo yatakayotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa Halmashauri husika. 
Lakini, “kama Tume watachelewa kutoa idadi ya Viti Maalum katika Halmashauri husika, Mkutano Mkuu wa BAWACHA ngazi ya Wilaya utachagua Madiwani wa Viti Maalum kulingana na Kata zilizopo,” unasema mwongozo.
Mwongozo huo, unaonyesha mtiririko ufuatao katika mchakato wa kuwapata wagombea wa udiwani wa viti maalum:
Kwanza, Katibu wa BAWACHA wa Jimbo atachambua fomu za wagombea waliojitokeza. Pili, taarifa ya uchambuzi wa Katibu wa BAWACHA Jimbo itawasilishwa kwenye kamati ya uchuchaji ya Jimbo/Wilaya.
Tatu, taarifa ya Kamati ya Uchujaji ya Jimbo/Wilaya itawasilishwa kwenye Mkutano Mkuu wa BAWACHA Wilaya kwa ajili ya kupiga kura. 
Nne, Katibu wa BAWACHA wa Jimbo atawasilisha taarifa ya matokeo ya Mkutano wa Mkuu wa BAWACHA wa Jimbo/Wilaya uliofanya uchaguzi wa madiwani wa Viti Maalum kwenye Kikao cha Kamati ya Utendaji ya Jimbo/Wilaya, kwa ajili ya uthibitisho.
Tano, Katibu wa Jimbo/Wilaya ataandika barua ya kuwasilisha matokeo ya uteuzi wa Viti Maalum kwa Mratibu wa Kanda kwa ajili ya kuyawasilisha kwenye ofisi ya Katibu Mkuu. Na sita, Katibu Mkuu atawasilisha majina ya Viti Maalum kwenye Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Monday 13 July 2015

Lowassa hakieleweki


Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa

KATIKA mazingira yanayoonesha Edward Ngoyai Lowassa kutojiamini, ameahirisha kukutana na waandishi wa habari katika dakika za mwisho. Anaandika Yusuph Katimba … (endelea).
Leo saa 5:00 asubuhi, Lowassa alitarajia kukutana na waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari nyumbani kwake Masaki, jijini Dar es Salaam ili kuzungumza nao.
Taarifa ya Lowassa kukutana na waandishi ilitolewa leo mapema kupitia kwa Katibu wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Nevile Meena.
Sababu za kuahirishwa kwa mkutano huo hazijatolewa ufafanuzi mpaka sasa na haijaelezwa ni lini na watu atafanya mkutano huo.
Lowassa ni miongoni mwa makada 38 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliorudisha fomu za kuomba ridhaa ya chama hicho kuteuliwa kugombea urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu.
Hata hivyo, jina lake lilikatwa katika hatua za awali hivyo kuibua kile kilichoitwa mgogoro kwa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho (NEC-CCM) hasa waliokuwa wakimuunga mkono.

Chanzo: Mwanahalisi

Sunday 12 July 2015

Wahitimu wa kidato cha nne waliochaguliwa kujiunga na stashahada ya elimu 2015/2016



Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa wamefanya uchaguzi wa wanafunzi kwenye mafunzo ya Ualimu kwa kozi za Stashahada ya Kawaida ya Elimu ya Msingi na Stashahada ya Kawaida ya Elimu ya Sekondari Sayansi na Hisabati ambayo yataendeshwa kwenye Chuo Kikuu cha Dodoma. Uchaguzi huu ni kwa wale wahitimu wa kidato cha nne kwa mwaka 2014 waliofaulu kwa daraja la Krediti na zaidi lakini hawakupangiwa kidato cha tano. Utaratibu wa kuripoti utatolewa na chuo husika punde watakapomaliza maandalizi ya kupokea wanafunzi hawa. Majina ya waliochaguliwa kujiunga na masomo kwa mwaka wa masomo 2015/2016 yameambatinishwa hapa.

Magufuli mgombea Urais CCM

Dk. John Pombe Magufuli
Dk. John Pombe Magufuli

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimempitisha Dk. John Pombe Magufuli kuwa mgombea urais kupitia chama hicho
Katika Mkutano Mkuu uliofanyika usiku wa kuamkia leo mjini Dodoma, Dk. Magufuli amechaguliwa kwa kura 2104 sawa na asilimia 87.08, akifuatiwa na Balozi Amina Salum Ali aliyepata kura 253 sawa na asilimia 10.4 na Asha-Rose Migiro aliyepata kura 59 sawa na asilimia 2.44702.
Jumla ya kura zilizopigwa kwenye Mkutano Mkuu wa CCM kumchagua Mgombea atakayepeperusha bendera ya CCM kwenye uchaguzi Mkuu wa 2015 ni kura 2422, kura zilizoharibika ni sita, kura halali walizopigiwa wagombea ni 2416.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya kikao hicho, Dk. Magufuli amepita kwa kura hizo kutokana na nguvu yake dhidi ya wagombea wengine.
“Hakukuwa na namna hapa kwa kuwa, wajumbe wanaamini katika mazingira haya magumu ya upinzani Dk. Magufuli anaaminika na kukubalika nje kuliko hawa wengine,” anasema mtoa taarifa na kuongeza;
“Baada ya kutemwa Membe (Bernard Membe) kwenye NEC kila mjumbe ambaye alikuwa upande wa Lowassa (Edward Lowassa) alipumua jambo lililomrahisishia Magufuli.”
Mkutano huo umehairishwa mpaka saa nne asubuhi, ambapo ndiyo muda ambao Dk. Magufuli ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Mashariki na Waziri wa Ujenzi atatangazwa rasmi kuwa mgombea wa Urais kupitia chama hicho.
Awali ndani ya ukumbi wa mkutano, kulidawa kuwepo kwa mpango wa wafuasi wa Lowassa kutaka kumpitisha Balozi Amina ili chama hicho kipate changamoto katika ‘kumuuza’ kwa wananchi ikiwa ni kulipiza kisasi kwa kukatwa mtu wao (Lowassa).
Katika Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya chama hicho, majina yaliyopitishwa yalikiwa ni Migiro, Magufuli, Balozi Amina, Membe na January Makamba.
Katika Halmashauri Kuu ya CCM yalipita majina matatu ya Dk. Magufuli, Dk. Migiro na Balozi Amina

Chanzo: Mwanahalisi

Saturday 11 July 2015

NEC yashangaza watu, Membe, Makamba Out

Wagombea watatu waliopitishwa na NEC, Kutoka kushoto ni Dk. John Magufuli , Amina Salum Ali na Dk. Asha-Rose Migiro
Wagombea watatu waliopitishwa na NEC, Kutoka kushoto ni Dk. John Magufuli , Amina Salum Ali na Dk. Asha-Rose Migiro

HALMASHAURI Kuu ya Taifa (NEC) imemaliza kazi yake ya kuteua majina matatu ya wagombea wa CCM, ambayo hayakutarajiwa na wengi. NEC imewatupa nje, wagombea Bernard Membe na Januari Makamba. Anaandika Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Waliopenya kwenye hatua ya tatu bora ya NEC ni Dk. John Magufuli, Dk. Asha Rose-Migiro na Balozi Amina Salum Ali, ambao watachuana kwenye Mkutano Mkuu wa CCM unatarajia kuanza muda huu.
Dk. Magufuli ni mbunge wa Chato na Waziri wa Ujenzi, Dk. Migiro ni mbunge wa kuteuliwa na Waziri wa Katiba na Sheria na Balozi Amina ni Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Tume ya Umoja wa Afrika kwenye Umoja wa Mataifa, Marekani.
Magufuli ndiye aliyeibuka kinara baada ya kupata kura 290, wakati nafasi ya pili ilichukuliwa na Balozi Amina aliyepata kura 284, nafasi ya tatu ilishikwa na Dk. Migiro aliyepata kura 280, wakati nafasi ya nne ilienda kwa Makamba aliyepata kura 124 na Membe aliambulia kura 120.
Wagombea hao watatu watachuana kwenye Mkutano Mkuu wa chama hicho kwa kupigiwa kura ili kumpata mmoja ambaye atapeperusha bendera ya CCM kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2015 uliopangwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.
Kikao hicho ambacho kilianza kwa hofu kutokana na wanaosadikika kuwa ni wapambe wa Edward Lowassa kuimba wimbo wa uliomtukuza mgombea wao kwa kusema “tuna imani na Lowassa” haukusimama hata alipokuwa anaingia ukumbini Mwenyekiti Kikwete, ambapo alishuhudia kisicho cha kawaida kikiendelea.
Pamoja na sintofahamu hiyo lakini wazee wastaafu walioingia ukumbini walikubaliana na tafrani hiyo ni marais na wenyeviti wastaafu Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa, makamu wenyeviti Amani Karume, John Malecela, Cleopa Msuya, Pius Msekwa na waziri mkuu mstaafu Dk. Salim Ahmed Salim.
Busara za wazee hao ndiyo zilizofanya kikao hicho kumalizika kwa amani na kuwapata wagombea watatu ambao wataenda kumtoa mgombea mmoja.

Chanzo: Mwanahalisi

MCHAKATO URAIS CCM: Lowassa akatwa


Dodoma. “Anakatwa, hakatwi” ndilo swali lililokuwa linaulizwa nchi nzima jana, lakini hatimaye Kamati Kuu ya CCM iliyokutana hadi usiku wa manane iliibuka na jibu kwamba Edward Lowassa amekatwa, huku kukiwa na wingu zito baada ya wajumbe watatu kupingana na uamuzi huo.
Muda mfupi baada ya kikao hicho, pamoja na kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alikataa kutaja majina yaliyopitishwa, akaunti ya Twitter ya CCM, iliwataja waliopitishwa kuwa ni Bernard Membe, Dk John Magufuli, Dk Asha Rose Migiro, January Makamba na Amina Salum Ali na kuwatupa wengine 33 akiwamo Lowassa.
“Kikao cha Kamati Kuu kimeisha salama. Kesho (leo) Halmashauri Kuu itakutana kuanzia saa 4:00 asubuhi,” alisema Nape baada ya kikao hicho.
Alipotakiwa kutaja majina ya makada watano waliopitishwa, Nape alisema: “Nimeambiwa mchakato bado unaendelea na kesho (leo) Halmashauri Kuu itakutana kuendelea na kazi. Kwa hiyo nawakaribisha kesho kuanzia saa 4:00 asubuhi mje mchukue picha, habari, karibu sana.” Mkutano Mkuu utafanyika saa nane mchana leo.”
Dakika chache baada ya kikao hicho kumalizika, wajumbe watatu wa Kamati Kuu, wakiongozwa na mbunge wa Songea Mjini, Dk Emmanuel Nchimbi waliitisha mkutano na waandishi wa habari na kueleza kuwa wanapinga uamuzi huo ambao hawakuutaja, wakidai kuwa si majina yote yaliyowasilishwa mbele ya kamati hiyo.
Dk Nchimbi, akiongozana na mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa na mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Sofia Simba waliwaeleza waandishi wa habari mara tu baada ya mkutano wa Kamati Kuu kuwa kikao hicho hakikufuata kanuni kwa kuwa majina machache yaliwasilishwa na hayakuhusisha mgombea anayekubalika.
Ingawa hawakumtaja mgombea huyo waliyesema anatajwa na wengi, wajumbe hao wanafahamika kuwa wanamuunga mkono Lowassa.
Baada ya kikao hicho taarifa za wagombea hao zilisambaa kwa kasi katika mitandao ya kijamii na mijadala ya wazi ilianza kuhusu uamuzi wa kumtosa Lowassa, ambaye alikuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Serikali ya Awamu ya Nne.
Mmoja wa makada watano waliopitishwa kwenye mchujo huo aliithibitishia Mwananchi kuwa jina lake limepita, lakini akasema hataki akaririwe na badala yake akamshauri mwandishi aangalie akaunti ya twitter ya CCM baada ya nusu saa.
Habari za jina la Lowassa kukatwa zilizagaa tangu jana asubuhi, ilipoelezwa kuwa CCM ilifanya majadiliano na wadau mbalimbali kuangalia jinsi ya kudhibiti watu wanaounga mkono baada ya kupata taarifa kuwa ameenguliwa.
Lowassa azua mjadala
Awali wakati Kamati Kuu ya CCM ikikutana jana usiku kupitisha majina ya makada watano walioomba kuwania urais, jina la Edward Lowassa ndilo lililotawala mijadala mingi kwenye mitandao ya kijamii, likiambatana na swali moja; amekatwa, hajakatwa?
Hali hiyo iliendelea zaidi jana usiku wakati CCM ilipotangaza mabadiliko ya tatu ya ratiba za vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu.
Watu wengi walikuwa wamefurika kwenye jengo la makao makuu ya CCM mjini hapa, maarufu kama White House na walioruhusiwa kuingia walikuwa waandishi wa habari na wajumbe wa Halmashauri Kuu na Mkutano Mkuu, ambao walikuwa wakifuata makabrasha na vitambulisho.
Mapema jana, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye aliwaambia waandishi wa habari kuwa kikao cha Kamati ya Maadili na Usalama ingekutana kuanzia saa 4:00 asubuhi na kufuatiwa na Kamati Kuu saa 8:00 mchana, lakini baadaye akatangaza mabadiliko mengine ambayo yalionyesha kuwa Kamati Kuu ingekutana kuanzia saa 10:00 jioni na Halmashauri Kuu baada ya futari.
Majira ya saa 2:00 usiku, Nape alitangaza kuwa kikao cha Kamati Kuu kingeanza muda huo na kwamba kingechukua muda mrefu na hivyo Halmashauri Kuu itakutana leo kuanzia saa 4:00 asubuhi na orodha ya makada watano waliopita kwenye mchujo itatangazwa muda huo.
Wakati Nape anawaambia waandishi wa habari jana asubuhi kuhusu sababu za kuahirishwa kwa vikao, tayari kulikuwa na habari kuwa Lowassa ameenguliwa baada ya vikao vya maridhiano kabla ya vikao hivyo vya juu kuhusu namna ya kudhibiti wanachama wanaomuunga mkono.
Habari hiyo ndiyo iliyokuwa mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii. “Amekatwa au hajakatwa?” ndilo swali lililoulizwa na wengi kwenye mitandao hiyo kutaka kujua kama kada huyo, aliyeonyesha kuungwa mkono na wengi wakati wa kusaka wadhamini.
Akizungumza na waandishi jana asubuhi, Nape alisema kuahirishwa kwa vikao hivyo muhimu kulitokana na mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete kuwa na vikao na watu mbalimbali kupata ushauri kuhusu namna ya kumaliza mchujo kwa usalama.
“Mwenyekiti alikuwa na vikao mbalimbali vya consultation (mashauriano) na wadau ili kuhakikisha vikao vinakwenda salama,” alisema Nape na kuongeza kuwa hiyo ndiyo ilisababisha ratiba ya vikao kubadilishwa.
Hata hivyo, Nape hakuelezea vikao vya mashauriano kati ya Rais Kikwete na Serikali vilihusisha makundi gani.
Nape alisema mabadiliko hayo pia yalitokana na shughuli za kiserikali na kichama ambazo Kikwete alikuwa nazo mjini Dodoma, ambako Julai 9 mwenyekiti huyo wa CCM alifanya kazi mbili za kuzindua jengo jipya la mikutano la chama hicho na baadaye kulihutubia kwa mara ya mwisho Bunge la 10, siku ambayo alitakiwa kuongoza kikao cha Kamati Kuu.
Awali Kamati ya Usalama na Maadili, ambayo inachambua wagombea na kutoa mapendekezo ya kila mmoja, ilipangwa kukutana Julai 8, na kufuatiwa na Kamati Kuu (Julai 9), Halmashauri Kuu ya Taifa (Julai 10) na Mkutano Mkuu ambao ungefanyika Julai 11-12.
Lowassa ndiye anayeonekana kuwa kinara miongoni mwa makada 38 walioomba kugombea urais kwa tiketi ya CCM, akionekana kuwa na wafuasi wengi ndani na nje ya chama, hali ambayo aliionyesha kwenye harakati za kutafuta wadhamini.
Mbunge huyo wa Monduli aliungwa mkono na takriban wenyeviti 15 wa mikoa, wabunge kadhaa waliojitokeza bayana kueleza misimamo yao kwake na wajumbe kadhaa wa Halmashauri Kuu na Mkutano Mkuu.
Jana, baada ya kusogezwa mbele kwa kikao cha Halmashauri Kuu, watu wengi waliondoka kwenye viwanja vya makao makuu ya CCM, na hakukuwapo na makada wanaowania kugombea urais kwenye eneo hilo ambako Kamati Kuu ilikuwa ikiendelea na kikao chake.
Kwa kawaida Kamati Kuu hupitisha majina matano kwa makubaliano licha ya kwamba katiba ya CCM inaruhusu maamuzi kufikiwa kwa kupiga kura.
“Mara nyingi hakuna upigaji kura kwenye vikao vya Kamati Kuu,” alisema Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Profesa Mark Mwandosya alipoongea na Mwananchi nje ya jengo hilo jana saa 2:40 usiku baada ya kuarifiwa kuwa kikao cha Halmashauri Kuu kimeahirishwa hadi leo.
“Mara nyingi uamuzi huwa ni kwa maridhiano licha ya Katiba kuruhusu upinzani kura pale mnaposhindwa kukubaliana,” alisema Profesa Mwandosya ambaye alikuwa mjumbe wa Kamati Kuu.

Chanzo: Mwananchi

Monday 6 July 2015

Kamata fursa ya biashara ya mtandao kwa mtaji wa 76500/=



Biashara ya mtandao( Network Marketing) nchini Tanzania imekuwepo kwa muda mrefu hivi sasa na mpaka sasa kuna makampuni zaidi ya 20 mpaka kufikia sasa,nyingi ya kampuni hizi zina bidhaa ambazo wengi wetu tumekuwa tukitumia kama virutubisho(Food supplements).

Lakini kampuni ya kipekee nchini Tanzania ambayo iko katika mfumo wa biashara wa mtandao kwa kutumia bidhaa isiyoshikika ni Rifaro Africa (www.rifaroafrica.com).


Bidhaa yake kubwa ni muda wa maongezi/hewani(airtime),hii ina maanisha kwa kila mtumiaji wa simu anayejiunga na kampuni hii ana nafasi ya kuwashirikisha watu wengine wajiunge nayo na kisha utapata nafasi ya kupata muda wa maongezi wenye thamani ya shilingi 10,000 kwa mara moja ambao utautumia kwa mwezi mzima(mfano leo utatumia 500,kesho 1000 mpaka siku 30 yaani  mwezi mzima na baada ya hapo utatununua muda wa maongezi kwa kutumia salio lako la kwenye simu yako ambalo utakuwa ukilipwa na kampuni kwa wiki na kwa mwezi baada ya kuwashirikisha watu wengine ambao watajiunga kwenye mfumo huu wa kampuni na kupewa namba ya uanachama(ID).


Kampuni ya Rifaro Africa imesajiliwa rasmi hapa Tanzania na kupewa hati zote kama kampuni binafsi inayoendesha biashara hii,pia ipo kwenye orodha ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) kwa kupewa namba maalumu ambayo ni 15420 ambayo baada ya kujiunga utakuwa na uwezo wa kujua timu yako imefikia idadi ya watu wangapi na pia kujua kipato chako kwa kutumia namba hiyo.


Mtaji wa kujiunga na biashara hii ni 76,500/= unaweza kuona ni nyingi lakini manufaa yake ni makubwa kulinganisha na faida ambayo utaenda kuipata kupitia mfumo wa biashara ya mtandao.

Ukilipia 76,500/= utapewa Vocha(airtime) yenye thamani ya sh.10,000/=,Kitabu cha biashara(Business manual),Laini ya simu na namba maalum ya uanachama(ID) na akaunti ya biashara.


Ukishajiunga, utapata TZS 10,000 kwa kila mtu utakayemshirikisha moja kwa moja kwenye kizazi chako cha kwanza, 

Utapata TZS 4,000 kwa kila mtu atakayeshirikishwa kwenye kizazi chako cha pili cha mtandao, 
Utapata TZS 2,000 kwa kila mtu atakayeshirikishwa kwenye kizazi chako cha tatu hadi cha tano,
Utapata TZS 1,000 kwa kila mtu atakayeshirikishwa kwenye kizazi chako cha sita hadi cha tisa.
Utapata tena TZS 2,000 kwa kizazi chako cha kumi.

Mapato haya yanalipwa kwa wiki kila siku ya Jumatano.


Tuangalie matarajio ya malipo kwa kualika watu watano tu (unaruhusiwa kualika watu wengi uwezavyo) ndani ya mwezi na hao watu watano wakaalika watu watano tu ndani ya mwezi huo huo kwa vizazi vitano tu kwenda chini. Mapato yako ya mwezi huo yatakuwa kama ifuatavyo kwenye mwezi husika:


TIMU YA WANACHAMA
MALIPO KWA KILA MTU KWA WIKI
JUMLA YA PESA
Kizazi cha 1 -Watu 5
         10,000 
               50,000 
Kizazi cha 2 -Watu 5X5=25
           4,000
             100,000
Kizazi cha 3 -Watu 25XX5=125
           2,000
             250,000
Kizazi cha 4 -Watu 125X5= 625
           2,000
         1,250,000
Kizazi cha 5 -Watu 625X5=3125
           2,000
         6,250,000
Jumla kuu kwa mwezi
         7,900,000


Mapato ya pili ni ya mwezi ambapo utalipwa 1% ya matumizi yako mwenyewe ya muda wa maongezi pamoja na matumizi  ya watu wa kizazi chako cha kumi.

Utalipwa 0.5% kwa matumizi ya kizazi cha pili hadi cha tisa.
Utapata mapato haya ya mwezi iwapo utatumia mda wa maongezi usiopungua TZS 10,000 katika mwezi husika, kitu ambacho wengi wetu tunakilipia na zaidi kwenye mawasiliano yetu ya mwezi na bila kupata malipo yoyote.

Tuchukulie una watu 10 kwenye kizazi chako cha kwanza ambao wamelipia kiwango cha chini cha TZS 10,000 cha manunuzi ya airtime kwa mwezi ambao nao wana watu 10 chini yao waliolipia hiki kiwango cha TZS 10,000 kwa vizazi vitano tu kwenda chini (Utalipwa mpaka vizazi kumi kwenda chini). Malipo yako ya mwezi yatakuwa kama ifuatavyo:

TIMU
MALIPO YA 0.5%
MAPATO YAKE
Kizazi cha 1= Watu 10
         100,000 
                 500 
Kizazi cha 2 (10X10)=Watu100
         1,000,000
                 5,000
Kizazi cha 3 (100X10)=Watu1000
         10,000,000
               50,000
Kizazi cha 4 (1000X10)=Watu10000
         100,000,000
             500,000
Kizazi cha 5 (10000X10)=Watu100000
         1,000,000,000
         5,000,000
Jumla kuu kwa mwezi
         5,556,000


Mbali na malipo haya kuna faida nyingine za malipo ambazo kampuni itakupatia endapo utakuwa una uwezo wa kufungua vituo vya Rifaro Africa kwa sehemu ambazo hakuna ofisi mfano mikoani ,Pia kwa mtu ambaye atakuwa amejiunga na kampuni hii na ameweza kusajili watu watano chini yake,atajaza fomu maalumu ambayo itamuwezesha laini yake kusajili watu kwa kutumia laini ya kampuni ya simu ambayo Rifaro wanafanya nayo kazi,hivyo simu yako itakuwa ikisajili laini zingine ambapo utalipwa mapato ya asilimia 20 kwa mwezi ya watumiaji wa simu ambazo utakuwa umesajili wewe kwa kipindi cha miezi mitatu na asilimia 10 kwa miezi mitatu itakayofuata jumla utafaidika kwa miezi sita kwa watumiaji wa simu utakaokuwa umewasajili kupitia laini yako.


Jamani hii ni fursa tosha kwa mtanzania,asiyeona hili basi anahitaji jicho la Tatu!! ndugu Mtanzania mwenzangu wasiliana nami ili ufike ofisini ujionee mwenyewe kwa wale wa mikoani tuwasiliane kwa simu na uatapata maelezo yote ya jinsi ya kujiunga uko uliko.

Kampuni ya simu iliyoingia mkataba na kampuni hii ya Kitanzania kusambaza bidhaa zake kwa njia ya mtandao imeridhia kufanya hivyo ili itumie pesa nyingi zinazotumika kulipia matangazo kwenye mabango, television, radio, magazeti, mitandaoni, n.k. kuwapatia wana mtandao ambao ndio watakaoeneza biashara yao kwa njia ya kuwadhamini watu wanaotaka kuingia kwenye biashara hii ya mtandao.

Kwa nini hii sio fursa ya kuiacha ikupite?

Kwanza mtandao huu umejikita katika kutoa huduma ya mawasiliano ambayo kila mtu hapa Tanzania anahitaji kwa shughuli zake za biashara.

Pili, kampuni husika ya mawasiliano ina huduma ya kupiga simu kwa gharama nafuu hivyo utapunguza mno gharama zako za mawasiliano ukiwa mtumiaji wa huduma za kampuni hii ukilinganisha na kampuni nyingine za mawasiliano.

Tatu mtandao huu ni mpya tofauti na mitandao mingi mingine hivyo una fursa kubwa ya kupata watu wa kujiunga nayo kwani wengi bado hawajajiunga na hii fursa.

Nne mtandao huu ni kampuni ya Kitanzania iliyosajiliwa hapa nyumbani hivyo italipa kodi na kulipatia taifa mapato.

Tano ni vizuri kuwa na utamaduni wa kupigia debe ubunifu unaotokea nyumbani na kuunga mkono kuliko kushabikia vitu vya nje tu kwani kama msemo wa kiswahili usemavyo, zimwi likujualo halikuli likakwisha.

Sita kampuni ya mawasiliano iliyoridhia kutumia njia ya mtandao ni kampuni kubwa hapa Tanzania yenye kufanya biashara ya uhakika. Kwa sababu hiyo, haitaruhusu kampuni ya kitapeli ifanye biashara yake kupitia huduma zake. 
Hivyo mtandao huu ni wa uhakika. Mara tu mtu akishajiunga chini yako basi utamuona palepale kwenye akaunti yako ya mtandaoni pamoja na mapato ulioingiza kupitia kwake.

Kilichofanyika hapa ni kwamba kampuni ya mawasiliano itaondoa gharama za matangazo kujitangaza ambazo ni kubwa mno hasa kwa makampuni ya mawasiliano kama tunavyoshuhudia mabango yao, kwenye magazeti, mitandaoni, n.k. 
Hivyo badala ya kampuni hii ya mawasiliano kumwaga pesa kwa ajili ya kujitangaza na kushindana kibiashara, hela hizo zinaingizwa katika mapato ya wana mtandao ambao wao wanasambaza biashara hii kwa njia ya mdomo kuwaambia ndugu na jamaa zao kuhusu fursa hii ya mtandao.

KWA MAELEZO ZAIDI PIGA SIMU 0777 571 856

Chanzo: http://rifaroafricateam.blogspot.com