Subscribe For Free Updates!

We'll not spam mate! We promise.

Saturday 4 July 2015

Muswada wa sheria ya watoa taarifa wapitishwa bungeni



Waziri wa katiba na sheria Dr. ASHA ROSE MIGIRO
Bunge la jamhuri ya muungano wa TANZANIA leo  limepitisha muswada wa sheria ya kuwalinda watoa taarifa za uhalifu na mashahidi wa mwaka 2015, ikiwa ni hatua ya kuongeza kasi ya kupambana na vitendo vya uhalifu na ubadhilifu mkubwa wa rasilimali za umma.

Akijibu hoja za  wabunge Kuhusu  baadhi ya vifungu vya muswada huo, waziri wa katiba na sheria Dr. ASHA ROSE MIGIRO amesema muswada huo ukiwa sheria utaboresha utawala bora katika sekta za umma na binafsi kwa kuzingatia sheria za nchi.

Kwa takribani siku tatu, bunge limekuwa katika mjadala mzito wa kupitia vifungu  vya muswada  wa sheria ya kuwalinda watoa taarifa na mashahidi wa mwaka 2015, na hatimaye kuupitisha leo.
Waziri wa katiba na sheria  Dr.ASHA ROSE MIGIRO amesema muswada huo mbali na kuwalinda watoa taarifa na mashahidi utachochea na kuboresha mfumo wa utawala bora kwa mujibu wa sheria za nchi.

Mbunge wa KASULU mjini MOSES MACHALI amependekeza kuongezwa kwa adhabu kali kwa watakaowafichua watoa taarifa na mashahidi ili kufanikisha malengo yaliyomo katika muswada huo.
Katika hatua nyingine Spika wa bunge ANNE MAKINDA alilazimika kusitisha tena shughuli za bunge baada ya wabunge wa kambi rasmi ya upinzani kugomea hatua ya Waziri wa nishati na Madini GEORGE SIMBACHAWENE kuendelea kuwasilisha bungeni Miswada mitatu ya shera ya usimamizi wa sekta ya mafuta na gesi.

Source: http://www.tbc.go.tz/